Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:57

Rais wa Sudan Kusini hatashiriki mkutano wa New York.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipohudhuria baraza kuu la Umoja wa mataifa New York, Septemba 2011.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipohudhuria baraza kuu la Umoja wa mataifa New York, Septemba 2011.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir hatahudhuria mkutano wa kwenye baraza kuu la Umoja wa mataifa baadaye mwezi huu ambao uliitishwa na katibu mkuu Ban Ki Moon ili kuimarisha mkataba wa Amani .

Waziri wa habari Michael Makuei amesema rais Kiir amemtuma makamu wake James Wani Igga ili kuiwakilisha serikali ya Sudan Kusini.

Vile vile Makuei pia ameongeza kuwa mwaliko huo ulitolewa kwa rais katika muda mfupi.Amesema ingwaje rais Kiir anachukulia mkutano wa umoja wa mataifa kuwa na umuhimu , hali huko Sudan Kusini ni muhimu zaidi.

“Rais Salva Kiir haendi kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja la Umoja wa mataifa kwasababu ameshamtuma makamu trais wake James Wani Igga kwenda na kuhudguria mkutano wa baraza kuu kama ilivyopangwa” alisema.

XS
SM
MD
LG