Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:04

Mwaka mmoja baada ya shambulizi la maduka ya Westgate Nairobi


Mamia ya waombolezi waklusanyika nje ya jengo la Westgate
Mamia ya waombolezi waklusanyika nje ya jengo la Westgate

Maelfu ya Wakenya walikusanyika katika maeneo mbali mbali ya jiji la Nairobi Juampili, kuwakumbuka karibu watu 67 walouliwa na washambulizi wa Kisomali wenye itikadi kali za kislamu katika maduka ya kifahari ya Westgate mjini Nairobi mwaka 2014.

Kenya imekua katika hali ya juu ya tahadhari kuadhimisha siku hiyo ya Septemba 21, huku wananchi wakiendelea kuwa na masuali juu ya shambulio hilo lililodumu siku nne, wakitaka kujua uchunguzi umefiuka wapi na nani hasa walohusika.

Katika eneo la Msitu Karura mjini Nairobi karibu watu 2,500, wengi kati yao ni walonusurika na shambulio hilo pamoja na familia zao, walihudhuria ibada iliyofanywa kwa pamoja na dini mbali mbali pamoja na kuzinduliwa mnara wa makumbusho yenye majina ya walofariki.

Mnara wa makumbusha wa waathiriwa wa Westgate
Mnara wa makumbusha wa waathiriwa wa Westgate

Katika tahariri iliyochapishwa na gazeti la Sunday Nation, Rais Uhuru Kenyatta ameapa kwamba nchi yake haitokubali kushindwa na Al Shabab.

"Tumepambana kwa nguvu kuwashinda magaidi na wahalifu wanaowalenga raia wasio na hatia wanaoishi Kenya. Tumeendelea kuwa makini na Somalia, ambako vikosi vyetu vya ulinzi vinaendelea kujitoa mhanga kuwashinda magaidi na wanaowafadhili," aliandika Rais Uhuru.

Katika maduka ya Westgate mamia ya watu walikusanyika pia kuwakumbuka walopoteza maisha yao na kutolewa wito kwa Wakenya kuwa na umoja katika vita dhidi ya ugaidi.

XS
SM
MD
LG