Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:02

Meneja wa zamani wa Uganda Cranes apewa miaka 10 jela


Christopher Mubiru meneja wa zamani wa Uganda Cranes, akiwa mahakamani
Christopher Mubiru meneja wa zamani wa Uganda Cranes, akiwa mahakamani

Mahakama moja nchini Uganda imemhukumu aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya kandanda Chris Mubiru, miaka 10 gerezani kuwalipa waathirika fidia ya shilingi milioni 50 kila mmoja kwa makosa ya kufanya ngono na wanaume.

Katika uamuzi wake, mbele ya mahakama iliyofurika, Jaji Flavia Nabakooza ameeleza kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani unatosha kuamini kwamba Chris Mubiru alikuwa na mazoea ya kufanya tendo la ngono na wanaume bila ya idhini yao, akiwemo mwaathiriwa Emmanuel Nyanzi.

Ripoti ya Kennes Bwire
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:24 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jaji Nabakooza pia ameeleza mahakama kwamba vipimo vilivyofanywa katika maabara ya serikali vimethibitisha kwamba vitu vilivyopatikana nyumbani kwake Mubiru yakiwemo mafuta na dawa za kutuliza maumivu, vinatumiwa na mashoga.

Mawakili wake Chris Mubiru wakiongozwa na Isaac Semakadde, wamesema watakata rufaa. "Mteja wetu Chris Mubiru hajaridhia uamuzi wa mahakama na ametomba tukate rufaa katika mahakama kuu ya uganda" amesema Semakadde

Jaji Nabakooza, ametumia ibara ya 145 sehemu ya (a) ya sheria za Uganda, yani penal code, kumhukumu Mubiru kwa makosa ya ushoga, lakini wakili wake Mubiru wanasema mahakama imekosea.

"Tumeona mahakama imekosea kabisa lakini leo siwezi kuzungumzia sana" aliongezea kusema Semakadde.

Mwenyekiti wa muungano wa wanaopinga ushoga nchini Uganda Muhubiri Solomon Male, ameelezea furaha yake baada ya hukumu hiyo.

“Nina furaha sana hii leo kwamba huyu jamaa ambaye ni shoga, Chris Mubiru, ambaye amekuwa akiwalenga wavulana wenye umri mdogo, wachezaji soka, vipaji vinavyochipuka, amehukumiwa miaka 10 gerezani na kuamurishwa kuwalipa waathiriwa fidia ya shilingi milioni 50. Ni kesi ya kihistoria, hasa katika nchi ambayo wabunge wamekuwa wakiwadanganya raia kwamba hakuna sheria kuwahukumu mashoga” amesema Male.

XS
SM
MD
LG