Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:06

Kenya yafunga shule zote za umma nchini.


Darasa likiwa tupu katika shule ya msingi ya St.Mary Nairobi, Kenya, Sept. 6, 2011, kwasababu ya mgomo wa walimu.
Darasa likiwa tupu katika shule ya msingi ya St.Mary Nairobi, Kenya, Sept. 6, 2011, kwasababu ya mgomo wa walimu.

Serikali ya Kenya imetangaza kufunga shule zote za msingi na sekondari nchini humo kuanzia Jumatatu ijayo kutokana na mgomo wa kitaifa wa walimu unaoendelea nchini humo.

Mgomo huo utaingia katika wiki ya nne Jumatatu na shule hizo zitafungwa kwa muda usiojulikana .

Ila serikali imetangaza mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne itaanza tarehe 12, Novemba na ile ya darasa la 8 itaanza tarehe 10 mwezi huo. Kwa maana hiyo mitihani itaendelea kama kawaida na haitaahirishwa kutokana na mgomo huo .

Na kabla ya serikali kufunga shule hizo mwenyekiti wa tume ya kuajiri walimu nchini Kenya ametangaza kusimamishwa kwa mishahara yote ya walimu wote wanaoshiriki kwenye mgomo huo, lakini mwenyekiti wa chama cha walimu nchini Kenya Bw. Nzilwa amewataka walimu hao wasiogope na waendelee kuwa ngangari na kumtaka mwenyekiti huyo aheshimu haki na sheria.

Hali ya elimu nchini Kenya bado inatatanisha lakini Waziri wa Elimu Leah Rotiuch amewataka walimu waendelee kuwasaidia wanafunzi wanaojindaa na mitihani yao kwa mwaka 2015.

Wakati huo huo upande wa upinzani umetoa wito wa kuondolewa madarakani kwa Rais Uhuru Kenyatta na kudai wanaandaa muswaada maalum wa kuhakaisha rais Kenyata anaondolewa madarakani na nafasi yake ichukuliwe na naibu rais William Rais William Ruto kwa muda uliosalia wa uongozi wa serikali ya muungano wa Jubilee.

XS
SM
MD
LG