Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 21:37

Kabila awafukuza kazi washirika wake wa serikali


Wafusai wa upinzani wa Congo wakiandamana Kinshasa JUmanne kupinga Kabila kubadili katiba
Wafusai wa upinzani wa Congo wakiandamana Kinshasa JUmanne kupinga Kabila kubadili katiba

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amewafukuza kazi wanasiasa saba waandamizi kutoka serikali yake ya mungano baada ya kumandikia barua kumtaka kuheshimu katiba na kuton'gan'gania madaraka.

Katika barua iliyochapishwa hadharani, viongozi hao walopewa jina la G7, wanalaani kile walichokieleza ni "mkakati wa kujitia kitanzi" wa Kabila kwa kujaribu kubaki madarakani.

Barua hiyo iliyochapishwa Jumatatu, inamtaka Kabila kutayarisha mabadiliko ya madaraka kufuatana na katiba na kuitisha uchaguzi kama ulivyopangwa.

Amri mbili alizotoa Rais Kabila Jumatano jioni, inamuondowa mshauri wake wa uslama Pierre Lumbi, kiongozi cha chama cha MSR, na waziri wa mipango na manedeleo Olivier Kamitatu, kiongozi wa chama cha ARC.

Mgawanyiko ulitokea Jumatano mchana, pale Baraza la kisiasa la Muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais lilipokua linakutana asubuhi, kujadili athari zinazotokana na barua hiyo ya kundi la G7, pale wanasiasa hao saba walipojiondowa kutoka mazungumzo hayo.

Hali ya kisiasa huko Jamhuri ya kidemokrasia imeanza kutia wasi wasi kulingana na wachambuzi wa mambo kutokana na watu kutofahamu msimamo wa Rais Kabila ikiwa atagombania tena kiti chake katika uchaguzi wa Novemba 2016 au la.

Siku ya Jumanne vyama 10 vya upinzani viliitisha mkutano wa hadhara mjini Kinshasa kupinga hatua ya kiongozi huyo kujaribu kubadili katiba ili kuendelea kubaki madarakani.

XS
SM
MD
LG