Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 18, 2021 Local time: 11:59

Polisi wapambana na wafuasi wa Mbabazi Uganda.


Waziri wa mkuu wa zamani wa Uganda kwenye mkutano huko Afrika kusini. Mei 9, 2013.

Polisi wamekuwa na wakati mgumu kuwatawanya wafuasi wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi katika siku ya nne ya ziara yake mashariki mwa Uganda, watu kadhaa wamejeruhiwa.

Wafuasi wa Mbabazi, wamekaidi hatua ya polisi kuwarushia mabomu ya machozi ili kuwatawanya katika mji wa Jinja, huku wakizingira barabara wakitaka Mbabazi akiwahutubia kinyume na agizo la polisi.

Walinzi wa Mbabazi pia walisukumana na polisi, ambapo polisi mmoja alipigwa kofi huku mlinzi wa Mbabazi akinyang'anywa bastola.

Uchaguzi mkuu nchini Uganda unatarajiwa kufanyika mwaka 2016 ambapo rais Yoweri Museveni ametangaza kugombea kwa muhula mwingine. Rais Museveni yuko madarakani tangu mwaka 1986.

Ona maoni (1)

mjadala huu umefungwa
XS
SM
MD
LG