Blog ya "issamichuzi.blogspot.com" mwezi wa Septemba imetimiza miaka kumi toka ilipoanza kufanya kazi, na ni blog ambayo inaelezwa kuchochea uandishi na kuanzishwa kwa blog nchini Tanzania.
Mwanzilishi na mmiliki wake Muhidin Issa Michuzi, amesema kuna mafanikio mengi ambayo ameyapata kwa kuanzisha blog hiyo laiki kubwa yeye anaona ni kukubalika kwake ndani na nje ya Tanzania. Blog ya Michuzi ambayo imejizolea mashabiki weki, inaelezwa kubadilisha namna vyombo vya habari vya Tanzania, vilivyokuwa vikifanya kazi kalba ya kuanzishwa kwake hasa katika ushirikishwaji wa hadhira.
Katika mahojiano na VOA Express, matangazo yanayoletwa na Sauti ya Amerika, Bwana Michuzi alisema japokuwa sheria ya mitandao iliyoanza kufanya kazi rasmi mwezi Septemba, nchini Tanzania, na kuelezwa kukandamiza uhuru wa kutoa na kupokea maoni, yeye haamini hilo.
Bwana Michuzi amesema "hakuna uhuru usio na mipaka," hasa hivi sasa ambapo kila mtu anaweza kuwa mtoa habari kutokana na kuwepo nyenzo nyingi za habari hasa mitandao ya kijamii.
Sikiliza mahojiano ya Muhidin Michuzi na Idd Ligongo wa Sauti ya Amerika.