Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:41

Shilole asema manjonjo yake ni kujitoa fahamu na Dimpoz aomba kupigiwa kura tuzo za Afrimma.


Wasanii wa Bongom Flava Ommy Dimpoz na Shilole .
Wasanii wa Bongom Flava Ommy Dimpoz na Shilole .

Mwanamuziki Zuwena Mohamed au maarufu kama Shilole amesema sakata la kufungiwa kwake ni matatizo ambayo yanaweza kumkuta mtu katika sehemu yake ya kazi, na kuongeza kuwa ni “ajali kazini”. Shilole amesema hali iliyomkuta imetokea tu kwa bahati mbaya lakini watu wameichukulia tofauti, akidai kwamba baadhi ya watu wanaokwenda kumwangalia kwenye matamasha yake wanaweza kuwa na malengo mengine, wakingoja bahati mbaya itokee wachukue hatua akiongeza kwamba watu wameichukulia tofauti kabisa lakini kama mama aliumia sana hilo lilipotokea.

Akisema anashukuru yamekwisha na alipoulizwa yamekwisha vipi alisema hilo jambo “bado lipo in bracket” na yeye hawezi kulizungumzia kuna muongeaji wa hilo na kwa sasa liko nje ya uwezo wake.

Kuhusu kuvutia wapenzi wake amesema yeye haimbi nyimbo za Celine Dion akisema yeye manjonjo yake ni kujitoa fahamu na anajua nini anachokifanya.

Naye Omari Nyembo maarufu kama “Dimpoz” amesifu wanamuziki wa Bongo Flava wa Tanzania hasa akizungumzia kuhusu kuteuliwa kwake na wanamuziki wengine wa nchi hiyo kwenye tuzo za Afrimma huko Houton Texas hapa Marekani mwezi oktoba mwaka huu.

Tanzania imeweza kuingiza wasanii 14 katika tuzo za mwaka huu za Afrimma nyuma ya Nigeria ikiwa na wasanii 16 , alipojibu swali kuhusu kufanana kwa muziki wa Tanzania alisema kwamba hilo ni suala la “trend” yaani muziki wao unavyokwenda na kukua au kufanana akitoa mfano wa Afrika kusini katika kwaito , Marekani katika hip hop kwani anaona kila mahala muziki unafanana kinachopishana ni ujumbe wa maneno tu.

Akieleza kuhusu ukosoaji huo alisema watanzania wanakosoa kizazi kipya lakini wamesahau muziki wa zamani kwa mfano “michiriku” yote ilikuwa ikifanana , taarabu na miduara haoni ikiwa na tofauti yeyote akisema kwamba watu wasikilize ujumbe na melody.

Ila hakuacha kukosoa pia akisema lawama zake anazipeleka kwa wanamuziki wanaoiga wanamuziki wenzao badala ya kuwa kama wao wenyewe, ili mtu akisikia anajua huyu ni fulani.

Kusikiliza mahojiano bofya hapa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:20:41 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG