Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:17

Wafuasi wa Mbabazi Watawanywa na Polisi Uganda


Polisi nchini Uganda, wametumia risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi, wakati wa mkutano wa kisiasa mashariki mwa nchi hiyo.
Hatua ya polisi inakuja siku moja baada ya tume ya uchaguzi kutisha kumzuia Mbabazi kufanya kampeni ikidai anavunja sheria licha ya tume hiyo na mkuu wa polisi kumruhusu kukutana na wafuasi wake hapo awali.
Jumatano polisi walizingira uwanja mkubwa wa Boma, mjini Soroti, alikokuwa amepanga Mbabazi, kuhutubia wafuasi wake.

Siku ya nzima ya Jumatano, umati mkubwa wa watu waliojitokeza kumlaki Mbabazi, ambapo wakiwa nje ya uwanja huo, waliimba nyimbo za kumsifu Mbabazi.

Kutokana na nyimbo hizo walisi walianza kuwatawanya wafuasi wa Mbabazi kwa kutumia risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi.

Hata hivyo mda mfupi baadaye, wafuasi hao walijikusanya tena na kukaidi amri ya polisi lakini Bw Mbabazi aliwaomba wafuasi wake wawe watulivu.

Tume ya uchaguzi imesema kwamba haitamruhusu Mbabazi kufanya mikutano, ikidai kwamba amevunja sheria.

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda, Jotham Telemwa, alisema kwamba.

"Anastahili kukumbushwa sasa. Tutamkumbusha kwamba anafanya makosa, akikaidi ushauri wetu. Afuate mwonozo wetu ulivyo katika sehemu ya tatu ya sheria zinazosimamia uchaguzi wa Urais, tutamzuia, tumkamate na tuone cha kufanya".

Tangu siku ya Jumatatu, Mbabazi amekuwa akivutia umati mkubwa wa watu katika mikutano yake, baadhi ya wafuasi wake wakijitokeza barabarani kumlaki na hata kumlazimisha kuwahutubia.
Ujumbe mkubwa wa Bw Mbabazi ni wa mabadiliko katika uongozi wa Uganda, kama alivyosema.
"Nadhani shida yao ni kwamba hawataki kuona tena umati mkubwa wa watu katika mikutano yangu kama walivyoshuhudia mjini Mbale na kapchorwa. kamanda wa polisi wa hapa ameniambia kwamba amepata amri kutoka Kampala kwamba nisifanye mkutano tena na kwamba atatutawanya. sikukubaliana naye kwa sababu najua sheria. mimi ni mwanasheria."
Mbabazi alipewa ruhusa na mkuu wa polisi na tume ya uchaguzi kufanya mikutano kote nchini Uganda.
Lakini tangu Jumatatu alipoanza kuvutia umati mkubwa wa watu, kumekuwepo minong'ono ndani ya chama tawala cha NRM ikitaka asimamishwe.
XS
SM
MD
LG