Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:10

Msemaji wa Upinzani Burundi Auwawa


Polisi akijaribu kudhibiti mmaandamano mjini Bujumbura mwezi Mei 2015
Polisi akijaribu kudhibiti mmaandamano mjini Bujumbura mwezi Mei 2015

Msemaji wa upinzani wa Burundi ameuliwa mjini Bujumbura wakati ghasia za kisiasa zikiongezeka na serikali kutochukua hatua zozote.

Patrice Gahungu, msemaji wa chama cha Union for Peace and Democracy (UPD), aliuliwa na watu wasojulikana usiku wa Jumatatu alipowasili nyumbani kwake,

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Bujumbura anaripoti kwamba mwili wa Gahungu ni moja kati ya miili minne iliyopatikana Jumanne asubuhi kutokana na mauwaji yanayofanywa na watu wasojulikana katika mji mkuu wa Bujumbura.

Mauwaji hayo yanazusha hofu, uvumi na mvutano ulokuwepo tangu uchaguzi wa utata ulomrudisha Rais Pierre Nkurunziza madarakani kwa mhula wa tatu.

Mjane wa Gahungu, Clemence Nsabiyimbona anasema, "hiyo ilikua ni mauwaji ya kisiasa kwa sababu hakuwa na matatizo na mtu yeyote. Katika nchi hii hivi sasa ukimpinga wzi wazi chama tawala na serikali , mara moja unakua adui na unastahili kuuliwa."

Rais wa UPD, Zedi Feruzi aliuliwa mwezi Mei wakati wa wiki kadhaa za ghasia zilizochochewa na uwamuzi wa Nkurunziza kugombania mhula wa tatu.

XS
SM
MD
LG