Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 23:06

Serikali ya Sudan Kusini kuwasilisha bungeni mkataba wa Amani.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kamanda wa waasi Riek Machar wakipeana nyaraka baada ya kusaini mkataba wa kusityisha mapigano chini ya usimamizi wa (IGAD) huko Ethiopia.

Serikali ya Sudan Kusini inasema itawasilisha kwenye bunge lake Jumanne mkataba wa amani ulioasainiwa mwezi uliopita kati ya serikali na waasi wanaomuunga mkono makamu rais Riek Machar ili kumaliza mzozo wa karibu miaka miwili.

Waziri wa habari Michael Makuei alisema baada ya kupokea nyaraka hiyo, bunge hilo litaunda kamati kutathmini na kupendekeza makubaliano ya mwisho katika kutekeleza mkataba huo. Waasi hao wamesha sema wanaweza kufanyia marekebisho mkataba huo Jumanne.

Makuei aliiamboa VOA Jumatatu lawama katika ucheleweshaji kwa upande wa serikali katika kupitisha makubaliano ziko kwa Jumuiya ya maendeleo ya kikanda (IGAD) ambayo imekuwa iikisimamia makubaliano hayo.

Amesema baada ya rais Salva Kiir kusaini makubaliano hayo Agosti 26 IGAD walichukua kurasa zilizobaki za nyaraka hiyo bila kumpa nafasi rais kuweka sahihi yake kwenye kurasa zote za nyaraka hizo.

XS
SM
MD
LG