Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:20

Watuhumiwa wa Shambulio la Garissa watatibiwa Gerezani


Watu wanaimba katika uwanja wa "Freedom Corner" Nairobi, April 14, 2015, kuwakumbuka waathiriwa wa shambulizi la chuo kikuu cha Garissa

Mahakama moja mjini Nairobi, Kenya imeahirishwa kwa mara nyingine kuanza kwa kesi ya washukiwa watano wanaohusishwa na mauaji ya katika chuo kikuu cha Garissa.

Hakimu Charity Oluoch alikata pia ombi mawakili wa watuhimiwa kuhamishwa kutoka gereza kuu la Kamiti kwenda kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi.

Washukiwa hao wanatuhumiwa kwa kutekeleza shambulio la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa hapo Aprili tarehe 2 mwaka huu, ambapo wanafunzi, wafanya-kazi wa chuo hicho na maafisa wa usalama 147 waliuliwa. Vijana hao Mohammed Ali Abikai, Hassan Edin, Sahal Diriye, Osman Abdi na Rashid Charles Mberero ambaye ni raia wa Tanzania, kwa takriban miezi mitano wamezuiliwa katika gereza la Kamiti –moja ya magereza makuu nchini Kenya.

Kupitia mawakili wao walitaka mahakama iwaruhusu kutibiwa katika hospitali kuu ya Kenyatta iliyo jijini Nairobi, lakini hakimu Charity Oluoch akaagiza watibiwe ndani ya gereza hilo la Kamiti.

Upande wa mashtaka unaowakilisha serikali katika kesi hiyo ulipinga ombi hilo ukisema gereza la Kamiti lina kituo cha kupata matibabu, na hapakuwa na haja kuwapeleka katika hospitali ya Kenyatta.

Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini Kenya pia inataka kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa kwa haraka, kwa sababu za kiusalama.

Wafanyakazi wa afya wakimsaidia muathiriwa wa shambulio la Garissa
Wafanyakazi wa afya wakimsaidia muathiriwa wa shambulio la Garissa

Kesi hiyo ambayo haijaanza kusikizwa itatajwa tena mahakamani Jumanne Septemba tarerehe 8, japo wote walikana mashtaka ya kuhusika na shambulio hilo la kigaidi

Zaidi ya mshahidi kumi wanatarajiwa kufika mahakamani na kutoa ushahidi, dhidi ya washukiwa hao wa shambulio baya zaidi la kigaidi nchini Kenya katika kipindi cha miaka 17.

Chuo kikuu cha Garissa kilifungwa muda mfupi baada ya shmbulio hilo lililohusishwa na wapiganaji wa Al-Shabaab.

Wanafunzi waionusurika walihamishwa kusomea katika vyuo vingine.

XS
SM
MD
LG