Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 17:02

Kenya yawika Bejing katika Michezo ya Riadha Duniani


China Athletics Worlds

Wanariadha wa Kenya wanaendelea kuwika katika Michezo ya 15 ya Riadha Duniani huko Bejing, ambapo siku ya Jumatano Julius Yego alinyakua medali ya dhahabu katika kurusha mkuki.

Julius Yego wa Kenya akirusha mkuki katika michezo ya 15 ya Riadha Duniani Bejing n
Julius Yego wa Kenya akirusha mkuki katika michezo ya 15 ya Riadha Duniani Bejing n

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 14 tangu bingwa wa dunia kurusha mkuki umbali wa mita 98.48 mwaka 2001, Yego alifanikiwa kurusha mkuki wake umbali wa mita 92.72, na kuwaacha bingwa wa Afrika Ihab Abdelrahman El Sayed wa Misri kunyakua fedha na bingwa wa dunia katika mchezo huo Tero Pitkamaki kutoka Finland kuondoka na shaba.

Katika siku hii ya tano, michuano mingine ya kusisimua ilikua ni mbiyo za mita 3000 kuruka viunzi wanawake, iliyoshuhudia ushindi wa Mkenya Hyvin Kiyeng Jepkemoi aliyetumia muda wa dakika 9:19:11. Habiba Ghiribi wa Tunisia alichukua nafasi ya pili akifuatwa na Gesa Felicitas Krause wa Ujerumani.

Wanawake waruka kiunzi katika mbiyo za mita 3000
Wanawake waruka kiunzi katika mbiyo za mita 3000

Katika mbiyo za mita 5000, Hagos Gebrhiwet wa Ethopia alinyakua dhahabu kwa kutumia muda wa dakika 13 sekunde 45 nae Ben True wa Marekani alichukua nafasi ya pili akifiatwa na Mkenya Edwin Cheruiyot Soi aliyeondoka na medali ya shaba.

Hapo siku ya Jumanne bingwa wa dunia katika mbiyo za mita 800 David Lekuta Rudisha wa Kenya alinyakua kwa mara nyingine tena medali ya dhahabu akitumia muda wa dakika 1:45:84. Ushindi huo uliondowa hofu kwamba bingwa huyo aliyeweka rikodi ya dunia katika mbiyo hizo huko London mwaka 2012 amerudi kwa nguvu baada ya kufanyiwa upasuwaji wa goti.

David Rudisha akiongoza kumaliza miyo za mita 800
David Rudisha akiongoza kumaliza miyo za mita 800

Licha ya matokeo hayo ya kusisimua ya Kenya kuna wanariadha wake wawili walopatikana na kukubali kutumia dawa za kuongeza nguvu wakati wa michuano hiyo ya Bejing.

Maafisa wa Shirikisho la Kimataifa la Riadha IAAF walitangaza Jumatano kwamba Joyce Zakary aliykimbia mbiyo za mita 400 na Koki Manunga aliyekimbia mbiyo za mita 400 kuruka viunzi, wameshitisha kushirik katika micehzo hiyo baada ya kupimwa na kupatikana wametumia dawa zilizopigwa marufuku.

Maafisa wa riadha wa Kenya wanasema uchunguzi zaidi utafanyika watakaporudi nyumbani.

Kwa wakati huu katika orodha ya medali, Kenya inaongoza ikiwa na medali 6 za dhahabu 3 za fedha na 2 za shaba ikiwa na jumla ya medali 11

XS
SM
MD
LG