Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:51

VOA yaanda Kongamano juu ya Mitandao ya Kijamii na Uchaguzi Tanzania


Washiriki katika Kongamano la VOA , mjini Dar Es salaam
Washiriki katika Kongamano la VOA , mjini Dar Es salaam

Sauti ya Amerika VOA inaendesha kongamano la changamoto za mitandao ya kijamii katika utangazaji mjini Dar es Salaam, katika hoteli ya Serena.

Kongamano hilo linahudhuriwa na wajumbe wa redio washirika wa VOA huko Tanzania kujadili jukumu la mitandao ya kijamii katika uchaguzi mkuu na jukumu lao katika kuwaelimisha wapiga kura.

Kongamano litafuatiwa na mkutano maalum na redio washirika kujadili namna ya kushirikiana zaidi katika siku zijazo. Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, VOA, Negussi Mengesha pamoja na Mwamoyo Hamza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili na Steve Ferri, mkuu wa kitengo cha Teknohama, ni miongoni mwa wanaohudhuria kongamano hilo.

XS
SM
MD
LG