Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:41

Ajali ya Ndege Indonesia Hakuna Aliyenusurika


Maafisa wa Indonesia wamesema Jumanne kwamba hakuna mtu aliyenusurika katika ajali ya ndege iliyotokea Jumapili mashariki mwa Indonesia.

Wafanyakazi wa uokozi walifika katika eneo la ajali ya ndege ya shirika la Trigana Air namba 267 katika jimbo la Papua kwa mara ya kwanza leo.

Kikosi cha wafanyakazi hao kilicheleweshwa na hali mbaya ya hewa ambapo kiliripoti kwamba ndege hiyo iliharibika kabisa.

Ndege hiyo aina ya TR 42-300 yenye mashine mbili na “pangaboi” ilitoweka kwenye chombo cha kuongozea ndege muda mfupi kabla ya muda uliopaswa kutua huko Oksibil baada ya safari fupi kutoka Jayapura.

XS
SM
MD
LG