Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:40

Ubalozi wa Marekani Cuba Wafunguliwa Rasmi


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, amehudhuria sherehe ya kufungua upya ubalozi wa Marekani nchini Cuba, Ijumaa, na kutoa heshima kwa bendera ya Marekani wakati ilipokuwa ikipandishwa mjini Havana, ambapo sherehe hizo zimemaliza miaka 54 ya uhusiano mbaya kati ya Marekani na Cuba.

Bwana Kerry alisema kwamba “hakika hili ni tukio la kukumbukwa, siku ya kuachilia mbali vikwazo vya zamani na kuweza kuona uwezekano mpya.”

Ikichukuliwa kwamba yeye ndiye waziri wa mambo ya nje wa kwanza wa Marekani toka 1954 kufika Cuba, Bw Kerry alisema “unajisikia kama upo nyumbani” katika ubalozi uliopo Havana. Alihutubia hadhira ya maafisa kutoka pande zote za serikali na kundi kubwa la watu waliofika kuhudhuia katika mji mkuu wa Cuba.

Watu waliofika hapo walisimama wima wakati nyimbo za taifa zilipokuwa zinapigwa wakati wa sherehe hiyo.

Kerry alizungumza katika uwa wa ubalozi huo pembeni ya bendera, huku akiangalia ubalozi uliopo ufukweni mwa bahari ya Caribbean nyuma yake. Alipongeza uamuzi wa mwaka jana wa Rais Barack Obama na Rais wa Cuba Raul Castro kurudisha uhusiano ulioharibika kutokana na vita baridi.

Bwana Kerry alisema “Rais Obama na Rais Castro walifanya uamuzi mzuri kusitisha kuwa wafungwa wa historia na kuangalia fursa za leo na kesho.”

Bwana Kerry aliambatana na baadhi ya wabunge wa Marekani na wastaafu watatu kutoka jeshi la Marekani ambao waliishusha bendera ya Marekani mara ya mwisho mjini Havana mnamo Januari ya mwaka 1961.

XS
SM
MD
LG