Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 18:14

Mgombea wa Urais wa CCM Achukuwa Fomu za Urais


Mgombea wa Urais wa CCM, John Magufuli na Mgombea Mwenza Samia Suluhu.
Mgombea wa Urais wa CCM, John Magufuli na Mgombea Mwenza Samia Suluhu.

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu leo wamechukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi NEC ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha Urais kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, nchini Tanzania.

Akizungumza na wafuasi na wapenzi wa CCM, jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama hicho Taifa Rais Jakaya Kikwete, amesema CCM, imejipanga katika nyanja zote ikiwemo sera na utekelezaji wa ilani ya chama hicho na kwamba ina uhakika wa kushinda uchaguzi mkuu ujao.Kwa upande wa mgombea urais wa chama hicho John Magufuli yeye ameahidi kutatua kero mbalimbali za Watanznaia, iwapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wagombea wengine wa vyama vya upinzani ambao tayari wamechukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi ni wa vyama vya UPDP, TLP, DP na CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA.

XS
SM
MD
LG