Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:27

Obama akamilisha ziara yake ya Kenya na Ethiopia


Rais Obama akiwa makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa Ethiopia.

Rais wa Marekani Barack Obama alimaliza ziara yake ya Kenya na Ethiopia Jumanne kwa kutoa hotuba zenye hamasa na changamoto katika bara la Afrika.

Katika hotuba yake kwa ziara hiyo ya kihistoria Rais Obama alipongeza maendeleo mazuri ya Afrika, huku akiyataja maendeleo hayo yanaweza kuendelea tu kupitia maendeleo endelevu na demokrasia kwa wote.

“Nina simama mbele yenu kwa fahari kama Mmarekani. Pia nasimama mbele yenu kama mtoto wa Mwafrika.” Ni maneno ya Rais Barack Obama, rais wa kwanza aliye madarakani wa Marekani kuhutubia Umoja wa Afrika, alielezea matarajio yake binafsi ya kuiona Afrika inaendelea kiuchumi, na ukuwaji wa maendeleo wakati ikiwa na kivuli cha historia ya ukoloni.

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

Pia alisema “Nusu karne katika kipindi hiki cha uhuru, ni kitu kilichopitwa na wakati kuendelea kuwa na mtazamo usio sahihi kwamba Afrika imegubikwa na umasikini na migogoro. Ulimwengu lazima utambue maendeleo makubwa ya Afrika.”

Bwana Obama alipongeza mafanikio ya bara la Afrika ambalo limepunguza maambikizi ya Ukimwi na HIV kwa mamilioni ya wa- Afrika ambao wameondolewa katika umasikini wakati tunaongoza nafasi ya Marekani katika maendeleo hayo.

Rais Obama alizungumzia pia juhudi za kukuza biashara na taasisi za Marekani zinazojishughulisha na kupambana na usalama wa chakula, kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa umeme, na kusaidia ujasiriamali wa Afrika.

Bila kuitaja China, bwana Obama alisisitiza kile kinachoiweka kando Marekani katika uwekezaji wake barani Afrika.

Rais Barack Obama akiwa kiwanda cha vyakula cha Faffa, Ethiopia
Rais Barack Obama akiwa kiwanda cha vyakula cha Faffa, Ethiopia

“Uhusiano wa kiuchumi hauwezi tu kuwa wa nchi nyingine kujenga miundo mbinu kwa kutumia wafanyakazi wa nje ama kwa kutumia rasilimali za Afrika. Ushirika wa kweli wa kiuchumi unapaswa kuwa mzuri pia kwa Afrika. Wanapaswa kutengeneza ajira na kuwajengea wa-Afrika uwezo.”

Lakini kiongozi wa Marekani alitahadharisha kuhusu maendeleo mazuri ya bara hilo yako katika msingi tete ambapo mamilioni ya wa-Afrika wakiwa bado wanaishi katika umasikini uliokithiri bila ya kuwa na miundo mbinu ya msingi.

Katika ujumbe wake ambao pia aliuzungumza katika ziara yake ya Kenya, Rais Obama aliainisha kwamba hakuna kitakacho fungua vichocheo vya uchumi wa Afrika bila kumaliza “saratani” ya rushwa.

“Kama mtu anapaswa kutoa rushwa kuanzisha biashara ama kwenda shule ama kumpata afisa kumfanyia kazi ambayo anapaswa kuifanya, hiyo sio hali ya ki-Afrika. Inakandamiza utu wa watu unaowawakilisha.”

Rais Barack Obama akiwa Ethiopia
Rais Barack Obama akiwa Ethiopia

Rais wa Marekani alifurahiwa sana wakati alipokuwa akizungumzia namna maendeleo ya Afrika yanavyotegemea demokrasia, ambayo amezungumzia si tu kwamba ya kufanya uchaguzi ulio rasmi. “Kama Wanahabari wanawekwa kizuizini kwa kufanya kazi yao, ama wanaharakati wanatishiwa wakati serikali zikipambana na asasi za kiraia, unaweza kuwa na demokrasia kwa jina tu, lakini si halisi.”

Hadhira iliyokuwa ikimsikiliza bwana Obama iliangua kicheko pale aliposema hawaelewi viongozi wa Afrika ambao wanakataa kuachia madaraka wakati vipindi vyao vinapokwisha, huku akielezea muda wake yeye unakaribia kufikia kikomo. “kwa mujibu wa katiba yetu siwezi kugombania tena. Siwezi kugombania. Na pia ninadhani kama nitagombea tena, nitaweza kushinda. Lakini siwezi.”

XS
SM
MD
LG