Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:16

Wafanyabiashara wadogo wanatumaini ziara ya Obama kuinua biashara zao.


Tangazo la biashara likimkartibisha Rais Obama nchini Kenya.
Tangazo la biashara likimkartibisha Rais Obama nchini Kenya.

Utafiti wa uchumi wa Kenya mwaka 2015 unaonyesha sekta isiyo rasmi iliajiri watu milioni 11.8 mwaka jana wanaofanya kazi katika sekta ya biashara ndogo ndogo ambazo mara nyingi hazina usimamizi . Mwandishi wa VOA, Lenny Ruvaga anamwangazia mfanyabiashara ndogo ndogo ya ufinyanzi katika sekta isiyo rasmi juu ya changamoto zake na kile anachotarajia kutokana na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama na mkutano wa kimataifa wa biashara duniani ambao Rais Obama atahudhuria .

Joseph Omondi anafanya kazi ya kutengeneza majiko ya mfinyanzi katika eneo la kutengeneza majiko kwenye karakana yake huko Korogocho nje kidogo ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Alianza kufanya kazi ya vyuma miaka minne iliyopita ili aweze kujisaidia mwenyewe na familia yake changa. Kila siku anatengeneza masufuria,mabakuli na masanduku ya vyuma. Kwa wastani biashara yake inampatia dola mia tatu kwa mwezi.

Akiwa mfanyakazi mwenye ujuzi wa hali ya chini ina maana kwamba Omondi hakuweza kuingiza kwenye soko rasmi la ajira . Kwa hiyo aliamua kuingia kwenye uzalishaji mdogo mdogo. Omondi ana matumaini kwamba mkutano huu wa biashara utasaidia biashara kama yake kupata fursa katika masoko ya kimataifa.

Anasema alipohojiwa kwamba "sala yangu ni kuwa na matumaini wakati Rais Obama atakuja atatupa ushauri jinsi gani wafanya biashara ndogo ndogo wanaweza kupata fursa ya kuingia katika soko la Marekani na hivyo tutakuwa tumeweza kufaidika na mkutano huo. Hili ndio tumaini langu".

Ripoti mpya kutoka tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika inasema Kenya ina sekta kubwa ya ajira isiyo rasmi barani Afrika kwa kiasi kikubwa kwa sababu uchumi ulio rasmi hauwezi kuajiri watu wote wanaotafuta kazi .Kiasi cha wakenya milioni 16 hawana ajira rasmi.

Ziara ya Obama, Kenya
Ziara ya Obama, Kenya

Serikali ina program za kuwasaidia vijana kupata mitaji inayohitajika kama vile mfuko wa biashara kwa vijana na mfuko wa uwezo ambayo inatoa mikopo kwa vijana na wanawake wanaoanzisha biashara bila riba.

Kwame Owino kutoka katika taasisi ya masuala ya kiuchumi (I.E.A) shirika la utafiti linalolenga uwajibikaji wa kifedha linasema msaada huo wa kibiashara unaweza kusaidia ufunguzi wa viwanda zaidi barani Afrika.

Anaeleza “hilo haliwezi kuepukika. Ikiwa sasa na kama hilo litatokea katika kila taifa kwenye bara la Afrika ni jambo tofauti kabisa kwa sababu kila nchi ina matatizo yake tofauti ya kisera ambayo yanahitaji kushughulikiwa lakini nafikiri ubunifu wa kibiashara unahitajika karibu bara zima la Afrika".

Mwishoni mwa wiki hii Kenya itakuwa mwenyeji wa mkutano wa dunia wa kibiashara ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Afrika katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na kusisitiza umuhimu wa biashara unaohitajika ili kuchochea ukuaji wa viwanda katika bara hilo.

XS
SM
MD
LG