Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:27

Watu wanane wauliwa katikia shambulizi la kituo cha polisi Dar


Majambazi wavamia kituo cha polisi Dar VOA mItaani
please wait

No media source currently available

0:00 0:07:37 0:00

Wakuu wa usalama mjini Dar es Salaam wamethinitisha Jumatatu kwamba kundi la karibu majambazi 20 walokuwa na silaha wameshambulia kituo cha polisi cha Stakishari Ukonga na kusababisha vifo vya polisi wanne na raia watatu na mshambuliaji mmoja.

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP- Ernest Mangu amethibitisha kutokea tukio hilo karibu saa nne usiku, lakini hakueleza wazi idadi ya silaha zilizoibiwa katika kituo hicho.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Amesema kufutatia tukio hilo jeshi la polisi limeanzisha Msako mkali dhidi ya watu waliovamia kituo hicho na kuwataka wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahusika wa tukio hilo.

“Tukio hili ni la kusikitisha na ni lazima tuchukuwe hatua kuwapata hawa walohusika. Mtakumbuka iliwahi kutokea tukio kama hili huko Ushiromb. Walivamia kituo kama hichi na ilisababisha pia mauwaji kwa askari. Basi sisi hatutachoka kupambana nao na tutahakikisha kwamba tutawapata.,” amesema Mangu.

Akizungumza Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadic na waandishi wa habari amelaani tukio hilo na kuwataka wananchi kushirikiana na vikosi vya usalama ili kuzuia matukio hayo .

Majirani wa kituo hicho katika mtaa wa Mugo Stakishari wanasema tukio hilo lilidumu zaidi ya Nusu saa huku milio ya risasi ikisikika kila kona hali iliyosababisha wanachi kujificha na kushindwa kutoa msaada wowote.

XS
SM
MD
LG