Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:05

Sudan Kusini yaadhimisha miaka minne ya uhuru.


Zulia jekundu liliwekwa siku ya kusheherekea uhuru wa Sudan Kusini.
Zulia jekundu liliwekwa siku ya kusheherekea uhuru wa Sudan Kusini.

Sudan Kusini inaadhimisha miaka minne ya uhuru wake, lakini kuna mambo machache ya kusheherekea wakati wananchi wakitaabika kutokana na mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe unaoendelea na kusababisha matatizo makubwa ya kibinadamu.

Raia wa Sudan Kusini wanalipa gharama ya vita ambavyo vilianza Disemba mwaka 2013 wakati mtafaruku wa kisiasa ulipotokea na kuingia katika ghasia za kisiasa, kati ya Rais Salva Kiir na mpinzani wake , makamu rais wa zamani Riek Machar.

Tangu wakati huo, maelfu ya watu wameuwawa, zaidi ya watu milioni mbili wamekoseshwa makazi na mamilioni zaidi wanakabiliwa na ukosefu wa chakula.

Mchambuzi wa sera, Nhial Tiitmamer wa taasisi ya Sudd mjini Juba anasema kuna fikra mchanganyiko wakati nchi hiyo ikiadhimisha uhuru ilioupigania vikali kutoka Sudan.

Uchumi wa Sudan Kusini ambao unategemea uuzaji mafuta nje ya nchi umeyumba vibaya na mgogoro na kuanguka kwa bei ya mafuta duniani kote.

Tiitmamer anasema hapa ndio mahali watu katika mji mkuu wanajihisi ndio waathirika wakubwa.

Pande zote mbili zinashutumiwa kwa kuhusika na ukiukaji wa haki wakati wa mgogoro ikiwemo watoto kulazimishwa kupatiwa mafunzo ya vita na unyanyasaji wa ngono kwa watoto.

Watu wasiopungua 150,000 wanapatiwa hifadhi ya ukimbizi kwenye eneo la Umoja wa Mataifa nchini humo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema matumaini yapo kidogo kwa Sudan Kusini. Alitoa wito kwa Rais Kiir na mpinzani wake Machar kuonyesha uongozi wao kwa kutafuta suluhisho la kisiasa nchini humo.

Katika ujumbe uliorekodiwa kwenda kwa watu wa Sudan Kusini, mshauri wa usalama wa taifa nchini Marekani, Susan Riice, amesema amevunjika moyo kuona kile kinachotokea Sudan Kusini. Ameweka lawama zote kwa viongozi wa nchi hiyo. Hapo jana Rais Kiir alianza muhula mpya wa miaka mitatu madarakani baada ya wabunge kupiga kura ya kuongeza muda wake wa uongozi.

XS
SM
MD
LG