Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:14

Rais Kikwete Afunga Bunge la Tanzania


Rais Jakaya Kikwete, wa Tanzania, amevihimiza vyama vya siasa nchini kuweka ahadi ya kuwezesha uchaguzi mkuu uendeshwe kwa uhuru na haki, kwa kuzingatia vyama hivyo ndio wadau wakubwa wa uchaguzi.

Rais Kikwete ameitoa rai hiyo wakati alipokuwa akilihutubia bunge la kumi mjini Dododma, ambalo limemaliza muda wake, ili kupisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Aidha, Rais Kikwete, alichukua wasaa kueleza mafanikio mbalimbali ambayo serikali imeyapata kwa kipindi cha miaka kumi ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya rushwa, ambapo watumishi wa serikali zaidi ya 90 wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa huku kiasi cha shilingi bilioni 80 kimeokolewa.

Pamoja na mambo mengine, Rais Jakaya Kikwete, ameeleza juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kudhibiti ujambazi, kuimarisha muungano, kupunguza ujangili wa wanyamapori na kuwepo kwa hali nzuri ya kisiasa visiwani Zanzibar, na akatoa matumaini yake kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana yataendelezwa na serikali ijayo.

XS
SM
MD
LG