Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:30

Mawaziri wa Zamani wa Tanzania Wahukumiwa Kwenda Gerezani


Mawaziri wa zamani wa Tanzania Basil Mramba na Daniel Yona wakiwa mahakamani
Mawaziri wa zamani wa Tanzania Basil Mramba na Daniel Yona wakiwa mahakamani

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, nchini Tanzania imewahukumu kwenda gerezani miaka mitatu na faini ya milioni tano kila mmoja, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basili Mramba, na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Pamoja na kwamba alikuwa katika kesi hiyo, mahakama hiyo imemuachia huru aliyekuwa Katibu mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

Hukumu hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu imetolewa na Hakimu Sam Rumanyika, wa mahakama hiyo.

Viongozi hao wa zamani katika serikali ya rais Benjamin Mkapa, walikuwa wanashtakiwa kwa pamoja kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 kwa kusamehe kodi kampuni ya Alex Stewart ya Uingereza.

XS
SM
MD
LG