Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 14:31

Ugiriki kufungua baadhi ya matawi ya benki.


Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras kwenye kikao cha bunge huko Athens, Ugiriki, June 28, 2015.

Benki za Ugiriki bado zimefungwa hii Jumanne wakati nchi hiyo ikionekana kuwa katika hali ya kutoweza kulipa sehemu ya mkopo wa dola bilioni 1.8 kutoka shirika la fedha duniani -IMF.

Wakati mustakabali wa kiuchumi wa nchi hiyo ikiwa haijulikani ilipofikia mapema Jumanne, wizara ya fedha ya Ugiriki imesema itafungua matawi yapatayo 1,000 ya benki kote nchini humo ili kuwawezesha wastaafu wengi wao wasio na kadi za benki –ATM kuweza kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya wiki nzima.

Wagiriki wanatarajiwa kupiga kura Julai 5 katika kura ya maoni juu ya duru mpya ya hatua za kubana matumizi ya Umoja wa Ulaya suala ambalo waziri mkuu Alexis Tsiparis anapinga.

XS
SM
MD
LG