Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 21:57

Umoja wa Ulaya umedhamiria kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa Burundi .


Ghasia za wananchi na polisi Burundi.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi walitoa kitisho kwa watu wanaojihusisha na ghasia za Burundi.

Umoja wa Ulaya umedhamiria kuchukua wajibu kama ikibidi kuchukua hatua za vikwazo kwa wale ambao vitendo vyao viliweza kupelekea au kusababisha ghasia na ukandamizaji ikiwa ni ukiukaji wa hali ya juu wa haki za binadamu. Walisema hayo baada ya mkutano huko Luxemburg.

Walimtaka mkuu wa sera wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini kuanza kazi ya maandalizi kwa uwezekano wa kuweka vikwazo dhidi ya watu katika taifa hilo la Afrika ya kati lililo matatani.

Mawaziri hao pia wamelaani kukwama kisiasa na kuzorota kwa hali ya usalama huko Burundi na kusema kuwa kutakuwa na kusema kwamba inapelekea hali mbaya kwa wakazi wa nchi na kwa kanda yote.

XS
SM
MD
LG