Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:44

Mali Yafikia Makubaliano ya Amani


Wapiganaji wa moja ya vikundi vyenye silaha nchini Mali.
Wapiganaji wa moja ya vikundi vyenye silaha nchini Mali.

Uongozi wa rais Barack Obama, wa Marekani umewapongeza watu wa Mali kufikia makubaliano ya amani yaliyowekwa saini baina ya waasi wa Tuareg na serikali.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje amesema Marekani, itasimama pamoja na watu wa Mali wakati wanatekeleza mpango huo kwa kuwaletea watu wa Mali amani na uthabiti wanaostahili kwa wakati ujao.

Serikali na muungano wa wanamgambo watiifu waliweka saini ya mpango wa amani mwezi Mei.

Lakini waasi wa Tuareg na washirika wao walikataa kushiriki zaidi katika makubaliano ya amani.

Makubaliano hayo ya amani yalifikiwa nchini Aljeria.

XS
SM
MD
LG