Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:51

Polisi wawili wafariki 9 wajeruhiwa Burundi


Polisi wajaribu kuwatawanya waandamanaji mjini Bujumbura
Polisi wajaribu kuwatawanya waandamanaji mjini Bujumbura

Polisi wawili wa Burundi wanaaminika wamefariki kutokana na majeraha walopata baada ya kushambuliwa kwa gruneti au risasi Ijuma usiku mjini Bujumbura.

Maafisa wa usalama hawajatoa taarifa yeyote kuhusiana na mfululizo wa mashambulizi yaliyotokea mitaa ya kaskazini ya Bujumbura, dhidi ya vituo vya polisi na magari yao.

Maafisa 11 walijeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo na wawili kati yao wanaripotoiwa walifariki katika hospitali ya kijeshi mjini Bujumbura siku ya Jumamosi.

Vyanzo vinaieleza Sauti ya Amerika kwamba, mashambulizi yalitokea katika mitaa iliyoshuhudia maandamano mengi katika mji huo, tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kugombania kiti chake kwa mhula wa tatu mwezi wa April.

Polisi imewalaumu wanaharakati wa upinzani kwa mashambulizi hayo,

XS
SM
MD
LG