Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:35

Vatican yahimiza watu kulinda mazingira


Picha ya Baba Mtakatifu Francis

Baba mtakatifu anasema anamuomba kila mtu kuipokea taarifa hii, ambayo kwa nia safi, ipo kwenye jukwaa moja na msimamo wa kanisa katika masuala ya kijamii.

Vatican ilitowa taarifa jana kutoka kwa baba mtakatifu Francis, akieleza kwamba mabadiliko ya hali ya hewa kwa kiasi kikubwa imechangiwa na vitendo vya binadam na kusema kuwa suala hilo ni mojawapo ya suala muhimu hii leo.

Taarifa hiyo ilotolewa jana yenye kurasa 191 , ilieleza kuwa ushahidi thabiti wa kisayansi, unaashiria kuwa tunashuhudia hali ya mabadiliko ya hali ya hewa inotia wasiwasi.

Akizungumza mbele ya umati wa watu nje ya Vatican jumatano, baba mtakatifu Francis alihimiza watu, kuwa na mtazamo wa wazi kwa taarifa hiyo.

Baba mtakatifu alisema,hii nyumba yetu inaharibiwa, na hilo linamuathiri kila mtu, hasa watu masikini. Huu ni wito wangu kwa jukumu kuchukuliwa, kulingana na jukumu mungu alilowapa binadam alipowaumba. Lima na litunze bustani ambalo aliwekwa binadam alipoumbwa. Ninamuomba kila mtu kuipokea taarifa hii, ambayo kwa nia safi, ipo kwenye jukwaa moja na msimamo wa kanisa katika masuala ya kijamii.

Kwenye mkutano wa jana, kadinal Peter Turkson aliorodhesha njia ambazo taarifa hio inalingana moja kwa moja na maadili ya kanisa.

Kadinali Turkson alisema kwamba ,kwa mfano uhusiano wa ndani baina ya masikini na udhaifu wa sayara , Imani kuwa kila kitu duniani kinahusiana, ukosoaji wa dhana mpya na mifano ya nguvu zitakazoibuka kutokana na technologia, mualiko wa kutazamia njia mbadala za kufafanua uchumi na maendeleo, thamani sahihi ya kila kiumbe, na maana ya ikologia yenye utu.

Kadhalika kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, profesa Hohn Schnellhuber, mwanzilishi na mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa athari ya hali ya hewa, ya Postdam , ambaye alisema hii ni sayansi imara, na waraka huo unakubaliana na ushahidi wa kisayansi.

Waraka huo, ambao ni waraka wa pili kwa ukubwa ambao papa anaweza kutowa, unakuja kabla ya ziara ya baba mtakatifu hapa Marekani hapo mwezi September, na kadhalika mkutano mkuu wa umoja mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mjini Paris baadae mwaka huu.

Msimamo wa baba mtakatifu Francis juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, unaonekana kuwa tofauti na msimamo wa hadhara ambao watangulizi wake walichukuwa na unatarajiwa kuwaudhi baadhi ya watu – hasa wenye sera za ki-consertive katika baadhi ya nchi.

XS
SM
MD
LG