Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:20

Timu ya Golden state Warriors yachukua ubingwa wa NBA .


Timu ya basketball ya Golden state Warriors ikishangilia ushindi.
Timu ya basketball ya Golden state Warriors ikishangilia ushindi.

Timu ya Golden State Warriors imeifunga Cleveland Cavaliers 107-95 Jumanne na kuchukua ubingwa wa michuano ya ligi wa mpira wa kikapu Marekani (NBA) kwa mwaka 2014-15.

Warriors walipata pointi 25 kila moja kutoka kwa Stephen Curry, mchezaji bora (MVP ) wa michuano ya ligi hiyo na Andre Iguodala na kusaidia timu hiyo kushinda katika mchezo huo kwa jumla ya michezo 4-2 ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1975. Iguodala ambaye katika msimu mzima amekuwa akicheza kama mchezaji wa akiba mpaka mchezo wa nne na Cleveland ambapo timu yake ilikuwa nyuma 2-1 alitangazwa mchezaji wa bora wa fainali hizo.

Mchezaji nyota wa Cleveland LeBron James aliongoza Cavaliers akiwa na pointi 32 , riboundi 18 na usaidizi 9 akionyesha umahiri mkubwa katika mchezo huo.Lakini Lebron alikuwa akicheza bila usaidizi wa nyota wenzake Kevin Love ambaye aliumizwa katika mechi za awali za mtoano na Kyrie Irving ,ambaye aliumia goti katika mchezo wa kwanza wa fainali , na kuwaacha Cleveland bila mfungaji muhimu kupambana na timu kali ya Golden State ambapo walishinda mechi 67 katika michezo ya awali.

Kushindwa kwa timu hiyo kumekuwa ni maumivu makali kwa Lebron James mzaliwa wa Ohio ambaye alianzia kuchezea huko Cleveland na timu ya Cavaliers na kurudi mwaka jana bada ya kushinda ubingwa wa NBA mara mbili akiwa na Miami Heat. Na pia ni maumivu mengine kwa michezo kwa ujumla kwa washabiki wa michezo huko Cleveland ambao wamekaa kwa zaidi ya miaka 50 bila kushinda kombe la aina yeyote kutoka kwa timu zao zinazoshiriki michuano mbali mbali mikubwa Cavaliers, Browns wa ligi ya NFL na Indians wanaocheza ligi kuu ya Baseball.

XS
SM
MD
LG