Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:13

Mwana Familia ya Bush Atangaza Rasmi Kuwania Urais


Gavana wa zamani wa jimbo la Florida, Jeb Bush, mtoto na kaka wa marais wa zamani wa Marekani, ametangaza rasmi kuingia katika mbio za urais.

Bwana Bush, ametangaza nia yake jana Jumatatu, na kuwa mgombea wa 11 katika chama cha Republikan, huku ikitazamiwa wagombea wengi zaidi kujitokeza.

Wakati anatangaza nia yake hiyo, alishangiliwa na wafuasi wake mjini Miami, Florida, na kudai Marekani ipo katika muelekeo mbaya.

Amelaumu chama cha Demokrat, kwa kuifanya nchi kuwa ni ya kusimamiana, na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi.

Amesema kwamba Marekani inahitaji rais atakayekuwa tayari kusitisha utamaduni uliopo sasa Washington, na yeye ndiye anayestahili kuongoza.


XS
SM
MD
LG