Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:04

Eritrea Yapuuzia Ripoti ya Umoja wa Mataifa


Rais wa Iritrea, Isaias Afwerki
Rais wa Iritrea, Isaias Afwerki

Eritrea imepuuzia ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo inaishutumu nchi hiyo kwa matukio mfululizo ya uvunjivu wa haki za binadamu ulioenea kwa kiwango kikubwa.

Katika taarifa ya jana Jumanne, ya wizara ya mambo ya nje ya Eritreat, imeeleza kwamba ripoti ya Umoja wa Mataifa haina ukweli wowote na vigezo.

Inaeleza kwamba shutuma hizo ni muendelezo wa kampeni ya kisiasa inayodidimiza maendeleo ya Eritrea katika siasa, uchumi, na jamii, ikijumuisha eneo la haki za binadamu.

Makundi kama “Human Right Watch” yamekuwa yakiishutumu serikali ya Eritrea kwa kukandamiza watu wake.

XS
SM
MD
LG