Viongozi wa upinzani wa Burundi wanasema wanapinga ratiba mpya ya uchaguzi iliyopendekezwa na Tume ya Taifa ya Uchagzi, CENI, wakidai kwamba tume hiyo haina tena mamlaka ya kisheria kutoa mapendekezo kama hayo.
Alkizungumza na Sauti ya Amerika, msemaji wa chama cha upinzani cha UPD, Patrice Gahungu, anasema hawakushiriki katika mkutano uloitishwa kuzungumzia uchaguzi hapo Jumatatu kwa vile wanaamini tume ya uchaguzi haina tena mamlaka ya kisheria.
Tume hiyo haiwezi kuchukua maamuzi ya kisheria kwa vile wajumbe wake wawili wamejiuzulu na hivyo hawana mamlaka chini ya katiba. Wanachotaka kufanya ni kupanga namna ya kuiba kura," alisema Gahungu.
Zaidi ya hayo anasema uchaguzi hauwezi kufanyika hadi pale Rais Pierre Nkurunziza kujiondowa kutoka kinya'ganyiro cha uchaguzi kugombani mhula wa tatu. Na inabidi vijana wanamgabo wa chama tawala wapokonywe silaha na hali ya usalama idumishwe ili kuweze kufanyika uchaguzi wa huru na haki.
Wachambuzi wanasema kwa jinsi hali ilivyo huko Burundi sasa njia iliyobaki ni maridhiano na upatanishi. David Monda, mchambuzi wa masuala ya kisiasa hapa Marekani anasema, "kusipokuwa na upatanishi, tusemae kutoka Umoja wa Mataifa au mataifa jirani, huwenda kukawa tena na vita, vile vita vya kikabila huwenda vikazuka tena."