Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:29

Ikulu ya Marekani Yakosoa Seneti


Ikulu ya Marekani imekosoa baraza la Seneti kwa kushindwa kufikia muafaka kabla ya muda mwa mwisho kufikiwa wa sheria inayoruhusu idara za usalama wa taifa kunasa taarifa za simu.

Msemaji wa White House, Josh Ernest, amesema kushindwa huko kwa bunge kumeleta hatari kwa Marekani ambayo haikutakiwa kuwepo.

Amesema kushindwa kwa baraza la Seneti kuafikiana kwa ni jambo la hatari, kwa sheria hiyo ambayo iliwekwa toka shambulizi la kigaidi la Septemba 11, mwaka 2001.

Amesema kuna athari katika kile ambacho maafisa wa usalama wa taifa wanaweza kufanya kuiweka Marekani katika hali ya usalama, ambapo kwa sasa chombo hicho muhimu hakipo tena.

XS
SM
MD
LG