Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:26

Baraza la mahakimu limewasilisha mashitaka dhidi ya Polisi wa Baltimore.


Meya wa Baltimore Stephanie Rawlings-Blake akizungumza na waandishi wa habari huko Baltimore, Mei 1, 2015.
Meya wa Baltimore Stephanie Rawlings-Blake akizungumza na waandishi wa habari huko Baltimore, Mei 1, 2015.

Mwendesha mashitaka mkuu wa jimbo la Maryland hapa Marekani anasema maafisa wote sita wa Polisi wanaoshitakiwa kwa kifo cha kijana Mmarekani mweusi aliyefariki mikononi mwao wameshitakiwa na baraza kuu la mahakimu .

Mwanasheria mkuu wa jimbo Marilyn Mosbi alisema baraza kuu la mahakimu limeamuwa kwamba kuna sababu za kutosha za kuwafungulia mashitaka rasmi maafisa wa idara ya Polisi ya Baltimore kwa kumkamata Freddie Gray, ambaye alifariki dunia mwezi Aprili baada ya kujeruhiwa akiwa mikononi mwa Polisi.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi Mosby amesema baraza la mahakimu limewasilisha mashitaka kadhaa dhidi ya Polisi wote sita na kuthibitisha shitaka kubwa kuliko yote la kitendo cha mauaji bila ya kudhamiria dhidi ya dereva wa gari la Polisi lililomsafirisha Gray baada ya kukamatwa Ceaser Goodson.

XS
SM
MD
LG