Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:19

Mwaka mmoja baada ya wasichana wa Chibok, VOA yawakumbuka.


Jopo la majadiliano la mjadala wa Sauti ya Amerika wa tukio la kuwakumbuka wasichana wa Chibok kutoka kushoto mkurugenzi wa VOA David Ensor, mbunge wa Florida Frederica Wilson na mbunge wa Carlifornia Karen Bass, na mmoja wa wasichana waliotoroka Chibok Patience Bulus na wakili wa haki za binadamu Emmanuel Ogebe.
Jopo la majadiliano la mjadala wa Sauti ya Amerika wa tukio la kuwakumbuka wasichana wa Chibok kutoka kushoto mkurugenzi wa VOA David Ensor, mbunge wa Florida Frederica Wilson na mbunge wa Carlifornia Karen Bass, na mmoja wa wasichana waliotoroka Chibok Patience Bulus na wakili wa haki za binadamu Emmanuel Ogebe.

Zaidi ya watoto 200 wa shule huko Nigeria waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram bado hawajulikani walipo, na kukosekana kwao kuna athari kubwa kupita nyumbani kwao.

Lakini ni wazi hawajasahaulika kama jopo la majadiliano la mjadala wa Sauti ya Amerika Jumanne, lilivyothibitisha katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutekwa nyara wasichana hao.

Tukio hilo lililofanyika katika makao makuu ya Sauti ya Amerika (VOA) mjini Washington Dc limefanyika ikiwa ni mwaka mmoja tangu kundi hilo kuteka wasichana 276 kutoka shule moja ya sekondari ya serikali usiku kati ya Aprili 14 na 15.

Wabunge wawili wa Marekani waliongoza maadhimisho hayo wakiwa ni wazungumzaji wakuu katika mjadala huo nao ni Karen Bass wa Carlifornia na Frederica Wilson wa Florida.

“Watoto wote wanastahili kupata elimu duniani kote , watoto hawa walinyang’anywa haki yao ya elimu kwa sababu Boko Haram wanaamini elimu ya magharibi ni dhambi” alisema mbunge Frederica Wilson.

“Nina furaha mmoja wa wasichana hawa aliyetoroka yuko nasi hapa , nawapa pole sana wazazi waliopoteza watoto wao siku hiyo” alisema mbunge Karen Bass.

Naye muongoazaji mjadala huo Jamila Fagge mwandishi wa Idhaa ya Hausa ya VOA alisema “Nimefurahi sana tunaadhimisha siku hii kwa sababu mnajali.

Katika ukumbi wa VOA pia alikuwapo Patience Bulus mmoja wa wasichana waliofanikiwa kutoroka wanamgambo hao. Hivi sasa yeye ni mmoja wa wasichana 10 ambao wamepata nafasi ya kusoma hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG