Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 17:39

Saudi Arabia yatangaza mashambulizi Yemen


Waandamanaji wa Yemen

Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, anasema nchi yake imeanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya waasi wa kishiha nchini Yemen.

Balozi Adel al-Jubeir amewaambia waandishi wa habari Jumatano jioni kwamba, nchi yake itafanya lolote kulinda watu wa Yemen na kile alichokiita serikali halali.

Amesema waasi wa Haothis kila mara huchagua njia ya ghasia.

Ameongeza kwamba, Saudi Arabia, ilishauriana na Marekani, kabla ya kuanzisha mashambulizi ya anga lakini hakuna uhakika kama Marekani, inashiriki katika mpango huo.

Mataifa mengine ya guba pia yameungana katika oparesheni hiyo ya kijeshi.

Mataifa kadhaa ya ghuba yanayoshiriki ni Bahrain, Kuwait, Qatar, na umoja wa falme za Kiarabu na zilitowa taarifa ya pamoja na Saudi Arabia kwa kusema yanailinda Yemen dhidi ya uvamizi wa waasi wa Haouthis.

XS
SM
MD
LG