Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:17

Mamia ya watu watekwa ikiwa ni pamoja na watoto Nigeria.


Wapiganaji wa Boko Haram.AFP PHOTO.
Wapiganaji wa Boko Haram.AFP PHOTO.

Maafisa nchini Nigeria wanasema wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamewateka mamia ya watu, wakiwemo watoto wengi kutoka mji uliopo kwenye mpaka na Niger.

Msemaji wa serikali ya Nigeria, Mike Omeri ameliambia shirika la habari la associated press-AP kwamba wanamgambo waliwateka wakazi wa mji wa Damasak katika jimbo la Borno wakati wakiondoka kutoka kwenye mji mwanzoni mwa mwezi huu.

Omeri alisema kundi hilo la waislam wenye msimamo mkali lilikwenda kwenye shule ya msingi ya Damasak, na kuwafunga wanafunzi na waalimu na kisha kuwachukua. Msemaji huyo alisema hawezi kutoa idadi kamili ya watu waliotekwa, lakini wakazi katika eneo wanaeleza idadi inafikia zaidi ya watu 500.

XS
SM
MD
LG