Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 22, 2024 Local time: 19:53

Shambulizi la kujitoa muhanga lafanyika Libya


Picha ya Maktaba
Picha ya Maktaba

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliendesha gari lake mpaka kwenye kituo cha ukaguzi barabarani mjini Bengazi, Libya, na kuua takriban wanajeshi saba.

Ripoti moja inasema huwenda washambuliaji wawili wamehusika katika shambulizi hilo.

Mpaka sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo, lakini tetesi za haraka zinahusisha wanamgambo wa kiislam.

Wanamgambo hao wameshikilia mji mkuu wa Tripoli, na kuunda serikali pinzani na kulazimisha serikali inayotambulika kimataifa kwenda upande wa mashariki mwa nchi.

Ghasia za Jumanne zimefanyika wakati balozi maalum wa umoja wa mataifa nchini Libya, Bernardino Leon, kupendekeza kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa katika juhudi nyingine ya kumaliza machafuko.

XS
SM
MD
LG