Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:37

Kampuni za biashara Kenya zabuni fuko la kuhifadhi maji


លោកស្រី Hillary Rodham កើត​នៅ​ថ្ងៃ​ទី២៦ ខែ​តុលា ឆ្នាំ​១៩៤៧។ លោកស្រី​កើត​នៅ​ក្នុង​គ្រួសារ​ថ្នាក់​កណ្តាល​មួយ​នៅ​ Park Ridge ជាយ​ក្រុង Chicago។ 
លោកស្រី Hillary Rodham កើត​នៅ​ថ្ងៃ​ទី២៦ ខែ​តុលា ឆ្នាំ​១៩៤៧។ លោកស្រី​កើត​នៅ​ក្នុង​គ្រួសារ​ថ្នាក់​កណ្តាល​មួយ​នៅ​ Park Ridge ជាយ​ក្រុង Chicago។ 

Huko Kenya katika muungano wa kipekee wa kuunganisha pamoja maslahi ya biashara na kuhifadhi mazingira, fuko jipya la maji limeanzishwa lenye lengo la kulinda vizuri Zaidi chanzo kikuu cha maji ya Nairobi, , mto Tana.

Kwa kuwekeza katika kuhifadhi mazingira, mashirika makubwa, kama vile Coaca Cola, na East African Breweries, yanataraji kupata mavuno makubwa, hata kuwa ni mafanikio kwa pande zote mbili biashara na mazingira.

Jane Kabugi mwenye umri wa miaka 68 , anajitaarisha kwa msimu wa kupanda mbegu. Kwa miaka mitano sasa Jane amekuwa mkulima mdogo wa kukidhi mahitaji ya familia yake, akitumia kila kitu anachozalisha.

Lakini hilo limebadilika mnamo mwaka ulopita, kwa kutumia ufundi mpya wa kuzalisha chakula ziada, sasa Kabugi anauza chakula sokoni.

Yeye ni mmoja wa wakulima wa mashamba madogo takriban elfu 5 waliopo katika eneo la juu lajuu la mto Tana, ambao wananufaika kutokana na mafunzo ya miezi mitatu inayotolewa na mfuko wa Water Fund ili kuimarisha ufundi wa ukulima, kama vile kuweka matuta ili kuzuia momonyoko wa ardhi.

Fuko la kusafisha maji Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:18 0:00

Kabugi anasema wasiwasi mkubwa ni maji.

Momonyoko wa ardhi na upungufu wa huduma ya maji inaathiri biashara, wakulima na jami, na kadhalika kuongeza gharama.

Na hii ndio sababu makampuni 10, yakiongozwa na Nature Conservancy, yalibuni mradi wa Nairobi water Fund, ili kulinda kiini cha maji na maeneo ya hifadhi maji kando ya mito inayotowa huduma ya Maji kwa takriban watu millioni 9 wanaoishi mjini Nairobi.

Mojawapo ya lengo lao kuu ni Bwawa la Thika ambalo inakusanya maji kutoka mito iliopo karibu yake na kuhakikisha maji yanapatikana kwa urahisi kwa wakazi wa Nairobi.

Kwa kuimarisha mtindo wa kulima, Kabugi na wakulima wengineo wamepunguza mchanga kuingia kwenye mto Na hivyo kupunguza gharama za kusafisha maji yanapoingia kwenye bwawa la Thika.

Kampuni ya Coca Cola ni mojawapo ya makampuni yanayojihusisha na imechangia takriban dola elfu 150 kwenye mradi huo wa Water Fund. sehemu ya fedha hizo zinakwenda katika kutowa mafunzo kwa wakulima. kampuni hiyo ya vinywaji inatumia takriban cubic mita millioni 30 za maj kila mwezi.

Bob Okello, ni mkurugenzi wa masuala ya umma wa kampuni ya Coca Cola, anasema kulinda maeneo ya kukinga maji ina manufaa kwa biashara ya shirika hilo.

Kwa Jane Kabugi na wakulima wengineo manufaa ya mradi huo, tayari unawaletea mavuno makubwa na kujenga jamii.

XS
SM
MD
LG