Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:38

Zaidi ya hekta 3,000 zateketezwa na moto msitu wa Mau, Kenya.


Sehemu ya mlima Longonot Naivasha Kenya.

Zaidi ya hekta 3000 zimeteketezwa na moto katika msitu wa Mau Complex kutokana na hali ya kiangazi inayoikumba nchi ya Kenya.Hali hii imekuwa ikitokea tangu mwishoni mwa mwezi uliopita (Februari) na kupelekea maofisa wa misitu kutoa tahadhari kwamba idadi kubwa ya matukio ya moto imeripotiwa katika misitu.

Waziri wa Mazingira, Maji na Maliasili Prof. Judi Wakhungu alisema msitu wa Mau ambao ndio msitu mkubwa nchini Kenya na ambao ni chanzo cha maji kwa mito kumi na mbili katika maziwa yote yalioko katika bonde la Ufa (Rift Valley Lakes), ikiwa ni pamoja na Ziwa Victoria, chanzo cha Mto Nile.

"Tumefanya uchunguzi wetu na maafisa wetu wamegundua kwamba karibu hekta 3,000 zimeharibiwa na moto," alisema waziri.

Bi.Wakhungu aliongeza kuwa moto katika misitu ina madhara chungu nzima. Hii italeta madhara makubwa ikiwemo mabadiliko ya hali ya anga ambayo huchangia kwa kiangazi, baa la njaa na umaskini

Alisema kuwa wizara yake, maafisa na askari kutoka shirika la misitu nchini Kenya watahakikisha wanalinda misitu usiku na mchana ili kuona kwamba hakuna moto mpya unaoanzishwa na wafanyabiashara wa mkaa.

Waziri alizungumza mwishoni mwa juma katika Shule ya Msingi ya Ndabibi, Naivasha katika jimbo la Nakuru katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Misitu. Mada ya mwaka huu ni “Misitu na Mabadiliko ya hali ya Anga.”

Msikilizaji wetu Isaac Njenga kutoka Naivasha, Kenya, amechangia maelezo katika habari hii.

XS
SM
MD
LG