Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:38

Netanyahu apata ushindi katika uchaguzi wa bunge Israel


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasaloimia wafuasi wake katika makao makuu ya chama chake cha Likud Tel Aviv. JUmatano, March 18, 2015.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasaloimia wafuasi wake katika makao makuu ya chama chake cha Likud Tel Aviv. JUmatano, March 18, 2015.

Chama cha waziri mkuu Benjamin Netanyahu, Likud kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa Israel na kumwezesha kurudi madarakani kwa muhula wa nne.

Kukiwa na asili mia 90 za kura kwisha hesabiwa, Likud kimejipatia viti 30, kikifuatiwa na mungano wa Zionist Union kilichojipatia viti 24.

Bw Netanyahu ameshajitangaza mshindi kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema "Likud imepata ushindi licha ya upinzani mkubwa"

Hata hivyo viti 30 ni vichache kabisa kuweza kuunda serikali, kwani inahitajika viti 61 kati ya viti 120 vya bunge kuunda serikali. Hivi sasa Israel inaingia katika awamu ya majadiliano ya kuunda serikali ya mungano.

Uchunguzi wa maoni hadi siku ya uchaguzi ulionesha kwamba chama cha Netanyahu kitashindwa na wapinzani wake wa muungano wa Zionist Union.

Bw. Herzog mpinzani wake mkuu amempongeza kwa ushindi huo lakini kusema atazungumza na vyama vingine kuona ni aina gani ya serikali itaweza kuundwa.

XS
SM
MD
LG