Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:48

Mchuano bado mkali uchaguzi wa Israel


Wakati wa upigaji kura katika uchaguzi wa Israel
Wakati wa upigaji kura katika uchaguzi wa Israel

Wagombea wawili wakuu wa uchaguzi wa bunge la Israel, wanabashiri ni wao watakaounda serikali mpya, japokuwa uchunguzi wa maoni ulotolewa na vituo vya televisheni unaonyesha kuna ushindani mkali.

Waziri mkuu, Benjamin Netanyahu, anatarajia kutawala kipindi cha nne na amesha jitangazia ushindi wa chama chake cha Kikonsevativ cha Likud, kwa kuandika katika ukurasa wa Facebook, kwamba chama cha Likud, kimeshinda dhidi ya wapinzani wake.

Mpinzani wake Bwana Isaac Herzog, wa chama cha muungano cha Zionist, amesema kila kitu kipo wazi mpaka matokeo ya mwisho yatolewe.

Aliongeza kusema anataka kujua vyama vingine vimeshinda viti vingapi kabla ya kutazamia aina ya serikali watakayounda.

Vyama vyote vikuu vinatarajiwa kushinda viti vingi zaidi ya ilivyobashiriwa hapo awali.

XS
SM
MD
LG