Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 05:45

Marekani yapoteza mawasiliano na ndege yake Syria


Makao makuu ya wizara ya ulinzi na jeshi Marekani, Pentagon.
Makao makuu ya wizara ya ulinzi na jeshi Marekani, Pentagon.

Jeshi la Marekani, Jumanne, limesema limepoteza mawasiliano na ndege yake isiyo na rubani ambayo ilikuwa ikiendeshwa kutoka ardhini, lakini haukutolewa ushirikiano kama imetunguliwa.

Taarifa ya Pentagon, inakuja kufuatia chombo cha habari cha serikali ya Syria, kumesema majeshi ya serikali yametungua ndege hiyo ya Marekani iliyokuwa inafanya uchunguzi.

Shirika la habari SANA halikutoa habari zaidi ya tukio hilo lililotokea katika jimbo la Latika, mwambao wa bahari Mediterranean.

Kama taarifa ni za kweli itakuwa ndege ya kwanza ya Marekani kutunguliwa ndani ya Syria toka mashambulizi yanayoongozwa na Marekani dhidi ya Islamic State, yaongezwe kutoka Iraq mpaka Syria, mwezi September.

Wakati huohuo shirika la kufuatilia masuala ya haki za binadamu nchini Syria lenya makazi Uingereza, limeshutumu vikosi vya serikali ya Syria, kwa kudondosha mabomu ya gesi ya sumu katika mji wa Sarmin, jimboni Idlib.

Katika taarifa yake ya Jumanne shirika hilo limesema shambulizi hilo limeua watu sita wakiwemo watoto watatu na kuwadhuru darzeni.

XS
SM
MD
LG