Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:49

Mwanajeshi mstaafu wa Marekani ashutumiwa kujiunga na Islamic State


Picha ya Maktaba ikionyesha picha iliyochukuliwa kutoka ukurasa wa Twitter unaohusishwa na Islamic State.
Picha ya Maktaba ikionyesha picha iliyochukuliwa kutoka ukurasa wa Twitter unaohusishwa na Islamic State.

Mstaafu wa jeshi la anga la Marekani, anatuhumiwa kujaribu kuwapatia msaada wa taarifa wanamgambo wa kundi la Islamic State.

Taarifa ya wizara ya sheria ya Marekani, inasema baraza kuu la mahakimu limemfungulia mashtaka Tairod Nathan Webster Pugh, kwa makosa ya kuzuia utekelezaji wa uwamuzi wa mahakama.

Taarifa iliyotolewa Jumanne imemnukuu mwendesha mashitaka wa serikali kuu Loretta Lynch, akisema mtuhumiwa huyo aliyezaliwa na kukulia Marekani.

Lynch ameongeza, Pugh, anatuhumiwa kuisaliti nchi yake na kujaribu kusafiri hadi Syria, kujiunga na kundi la kigaidi.

Mtuhumiwa huyo alijaribu kujiunga na Islamic State, mapema mwaka huu ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kufukuzwa kazi yake ya ufundi wa ndege mashariki ya kati.

Anaelezwa alihudumia jeshi la anga akiwa mtaalam wa mfumo wa vifaa na baadaye kufanya kazi katika kampuni binafsi.

Akikutwa na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka 35 gerezani.

XS
SM
MD
LG