Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:14

Polisi ashitakiwa kwa mauaji katika maandamano


Picha ya Maktaba, polisi wakizuia maandamano Cairo, Misri.
Picha ya Maktaba, polisi wakizuia maandamano Cairo, Misri.

Mwendesha mashitaka wa serikali ya Misri alimfungulia mashitaka afisa wa polisi kwa tuhuma za kumpiga risasi mwanamke mmoja wakati wa maadamano ya amani katikati ya mji mkuu Cairo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, AFP, sehemu ya kifo cha Shaima Al-Sabbagh, ilirekodiwa katika mkanda wa video na ilimsababisha rais Abdel Fattah Al-Sisi, wa Misri kutamka hadharani kwamba aliyehusika lazima afikishe katika mamlaka za haki.

Al-sabbagh, alifariki kutokana na majeraha wakati polisi walijaribu kuwatawanya waandamanaji wachache katika kuadhimisha miaka mine ya mapinduzi ya Januari 25.

Watu waliandamana kukumbuka wenzao waliokufa wakati wa maadamano yaliyomuondoa madarakani rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak.

XS
SM
MD
LG