Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:14

Wafanyakazi wa Marekani katika Ebola sasa wafikia 15 waliorudishwa


Vyumba vya kutibu Ebola, nchini Marekani.
Vyumba vya kutibu Ebola, nchini Marekani.

Wafanyakazi wengine wanne wa Kimarekani wamesafirishwa kwenda Marekani kwa uangalizi kufuatia uwezekano wa kuambukizwa virusi hatari vya Ebola.

Kutokana na wale waliowasili Jumanne, idadi ya wafanyakazi wa afya wa Marekani, waliorudishwa kutoka Sierra Leone, toka Ijumaa inafikia 15.

Maafisa wa Marekani, wamesema watu hao watewekwa katika uangalizi ndani ya vyumba maalum karibu na hospitali ya chuo kikuu cha Nebraska, taasisi ya taifa ya afya Maryland, ama hospitali ya chuo kikuu cha Emory, ya Atlanta, Georgia.

Vituo vyote vitatu vimetumika kutibu Ebola, siku za nyuma.

Kati ya wote hakuna aliyeonesha dalili za ugonjwa wa Ebola mpaka sasa.

Ebola imeshaua watu karibu 10,000 mpaka sasa nchini Sierra Leone, Liberia na Guinea.

XS
SM
MD
LG