Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:19

Afisa asema Marekani inapuuzia idadi ya wanajeshi wa kubaki Afghanistan


Picha ya Maktaba.
Picha ya Maktaba.

Afisa mmoja wa Marekani, anasema utawala wa rais Barack Obama, uantupilia mbali mpango wa kupunguza wanajeshi wa Marekani, nchini Afghanistan kufikia 5,500.

Pamoja na idadi hiyo kuwepo ifikiapo mwishoni mwa mwaka, maombi ya viongozi wa kijeshi yanataka kuwaweka wanajeshi zaidi nchini humo.

Japokuwa uamuzi wa mwisho wa idadi ya askari haujachukuliwa maafisa wanasema wengi kati ya karibu wanajeshi 10,000 ambao wapo nchini Afghanistan, wanatarajiwa kubaki vizuri kwa mwaka ujao.

Kuna uwezekano wa tangazo rasmi kutolewa wiki ijayo ambapo rais wa Afghan, Ashraf Ghani, atakutana na rais Barack Obama, mjini Washington.

Katika taarifa ya Jumatatu, ya Washington, msemaji wake Josh Ernest, hakutoa maoni yake kuhusu idadi lakini alisema rais aliwasiliana na timu yake ya usalama wa taifa na makamanda wake waliopo huko kuhusu hali halisi ya huko.

XS
SM
MD
LG