Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 16:22

Wapinzani waandamana Brazil kupinga rushwa


Maandamano Brazil dhidi ya Rais Rousseff
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:55 0:00

Karibu wafuasi milioni moja wa upinzani nchini Brazil, waliandamana katika miji mbalimbali nchini kote Jumapili, kutaka kuondoka kwa serikali ya rais Dilma Rouseff, kwa madai ya rushwa.

Hasira za waandamanaji wengi zililengwa dhidi ya Roussef, kwa ubadhirifu mkubwa katika kampuni ya taifa ya mafuta ya Petrobras.

Kampuni hiyo ya uchimbaji mafuta inayoendeswa na serikali ambayo imeshiriki katika kile waendesha mashitaka wanachokiita ulaji rushwa mkubwa kuwahi kutokea nchini Brazil.

Dola milioni 800 zilitolewa kwa hongo na fedha nyingine na kampuni kubwa ya ujenzi kubadilishana mikataba ya uchimbwaji mafuta.

Dazen ya wanasiasa wakiwemo washirika wa rais na viongozi wa Petrobras, wapo katika uchunguzi.

Hakuna aliyeshitakiwa kwa sasa lakini makamu 22, maseneta 13 na magavana wawili wamehusishwa na shutuma za uchukuwaji wa hongo.

Baadhi ya tuhuma zilitokea wakati Bi Rousseff akiwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Petrobras.

XS
SM
MD
LG