Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 22:05

Wanajeshi wa Iraq wasonga mbele licha ya upinzani wa ISIS


Mapambano yakiendelea kuelekea Tikrit

Majeshi ya Iraq, na wanamgambo wanaedelea kusonga mbele na mashambulizi kuelekea Tikrit, katika juhudi za kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa kundi la Islamic State.

Wapinzani wenye silaha na mabomu wamepunguza kasi ya mwelekeo wa wanajeshi na wapiganaji wa kujitolea wanaopigana kuelekea katikati ya ngome kubwa ya Islamic State kutoka pande mbili wiki hii.

Makamanda wa mashambulizi wanasema oparesheni iliyo katika wiki ya pili sasa inaendelea vizuri na kwa umadhubuti na kwa kukomboa maeneo zaidi.

Meja Jenerali mmoja ameliambia shirika la habari la kifaransa kwamba wamejikuta katika mapambano makali kwa sababu ya kukutana na mitego ya ardhini na walenga shabaha.

Kiongozi mmoja wa kundi kubwa la wanamgambo wa kishiha, Hali Al-Ameri, amesema wanamgambo waliopo Tikrit, wana mambo mawili ya kuchagua, kujisalimisha ama kufa.

XS
SM
MD
LG