Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 00:27

Ujerumani yatahadharisha kuipatia Ukraine silaha kali


Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika mapambano.

Mwanadiplomasia wa juu wa Ujerumani, ameonya dhidi ya kuipatia Ukraine, silaha kali katika mapambano dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Russia, akisema kwamba hatua hiyo itachochea uhasama wa hatari wa kudumu baina ya Kyiv na Moscow.

Waziri wa mashauri ya nje Frank Walter-Steinmeier, aliongea mjini Washington, Alhamisi baada ya mazungumzo na mwenzake wa Marekani, John Kerry.

Aliiambia hadhira katika kituo cha taaluma za kimataifa na mkakati kwamba kuipatia Ukraine, silaha hizo kutasababisha mgogoro huo ushamiri na kushindwa kuudhibitiwa.

Steinmeir pia alibashiri msukumo kutoka ndani na nje ya Marekani, wa kuipatia silaha Ukraine, utaongezeka endapo waasi watajaribu kuuteka mji muhimu wa kijeshi wa bandari wa Mariupol.

Tahadhari mpya ya Ujerumani, inatolewa siku kadhaa baada ya balozi wake wa Marekani, kusema bwana Barack Obama, amepinga Ukraine, kupewa silaha hizo kwa sasa.

XS
SM
MD
LG